Ibn Baaz kuhusu mwanaume kugusa kichwa cha mwanamke wakati wa matabano

Swali: Baadhi ya wafanya matabano huweka mkono juu ya kichwa cha mwanamke ambaye anamsomea. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Haidhuru ikiwa ni nyuma ya kizuizi. Ikiwa ni nyuma ya kizuizi kwa ajili ya kufanya kisomo kiwe imara. Ama kumgusa moja kwa moja hapana. Lakini ni sawa ikiwa anamsomea nyuma ya kizuizi, nyuma ya mtandio au nyuma ya ´Abaa´ah ambayo imefungwa vizuri ili kichwa kisitikisike.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24608/حكم-لمس-الرجل-راس-المراة-في-الرقية
  • Imechapishwa: 09/11/2024