Adhabu ya kwenda kwa mchawi ni mbaya zaidi kuliko ya mpiga ramli na kuhani

Swali: Ambaye anamwendea mchawi anapata adhabu sawa na ya ambaye anamwendea kuhani au mpiga ramli?

Jibu: Watawala wanatakiwa kuwazuia wote hao na wahakikishe watu hawawaendei wala hawawasadikishi. Ikibidi kuwatia adabu watiwe adabu. Mjinga afunzwe na ambaye anafanya makusudi atiwe adabu.

Swali: Adhabu ya ambaye anawaendea wachawi ndio adhabu hiyohiyo ya ambaye anawaendea makuhani?

Jibu: Ni mbaya na mbaya zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24610/ما-عقوبة-الذهاب-الى-الساحر
  • Imechapishwa: 09/11/2024