Swali: Yatosheleza kwa mwanamke kuswali nyumbani kwake kwa adhaana peke yake, au kwa adhaana na Iqaamah? Hali kadhalika mwanaume akichelewesha swalah yake na akaiswali nyumbani kwake, kinyume na wakati wake au katika wakati wake, inatosheleza kwake Iqaamah au ni lazima atoe adhaana na Iqaamah?
Jibu: Ama mwanaume inatosha kwake Iqaamah, kwa kuwa kishasikia adhaana. Wakati wa kuswali atakimu tu. Ama mwanamke, hana juu yake Iqaamah wala adhaana. Ni juu yake kuswali bila ya Iqaamah wala adhaana.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
- Imechapishwa: 01/02/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related

Mwanamke hana Adhaana wala Iqaamah
http://youtu.be/8gGnIz2BuhI Swali: Ikiwa ataadhini mwanamke nyumbani kwake, au mwalimu mwanamke madrasani kwake... Jibu: Hakuna adhaana kwa mwanamke. Mwanamke hakuwekewa katika Shari´ah adhaana wala Iqaamah.
In "´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan"

Adhaana na Iqaamah kwa mwenye kuswali peke yake
https://www.youtube.com/watch?v=uHr6XKaRakQ Swali: Wakati fulani nina swali (Swalah za) faradhi mimi mwenyewe kwa kutokuwa na Msikiti ulio karibu na mimi. Je, inanilazimu kwangu adhaana na Iqaamah katika kila Swalah au naweza kuziswali bila ya adhaana au bila ya Iqaamah? Jibu: Sunnah ni wewe uadhini na ukimi. Hii ndio Sunnah. Ama kuhusu…
In "Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz"
Mwanamke asiadhini na wala asikimu
Swali: Adhaana na Iqaamah imewekwa katika Shari´ah kwa wanawake? Jibu: Wanawake hawakuwekewa katika Shari´ah adhaana wala Iqaamah. Adhaana na Iqaamah ni kitu maalum kwa wanamme. Ama kuhusu mwanamke anatakiwa kuswali pasi na adhaana wala Iqaamah. Kwa msemo mwingine asiadhini na wala asikimu.
In "Adhaana ya mwanamke"