Amemkuta imamu katika safu ya mwisho na safu imejaa

Swali: Kuna mtu ameingia msikitini na akamkuta imamu yuko katika Tahiyyaat katika Rak´ah ya mwisho na safu imejaa. Je, akae chini na kuswali peke yake?

Jibu: Aswali peke yake.

Swali: Je, apange safu kwenye safu?

Jibu: Hapana, aswali peke yake.

Swali: Nakusudia kwamba asijiunge pamoja na wengine?

Jibu: Hapana. Asijiunge pamoja na mkusanyiko muda wa kuwa hakupata nafasi.

Swali: Endapo ataswali peke yake katika safu atalazimika kuirudia swalah yake?

Jibu: Ndio. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha kuirudia swalah yake aliyeswali peke yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22237/ما-يفعل-من-دخل-المسجد-والصفوف-مكتملة
  • Imechapishwa: 15/01/2023