Ibn Baaz kuhusu machinjio yanayotumia mashine katika kuchinja

Swali: Machinjioni hutaja jina la Allaah kwa yule mnyama wa kwanza na wanyama wengine hawatajiwi jina la Allaah.

Jibu: Inatosha kama amenuia wote.

Swali: Mchinjaji anayechinja kwa mashine anataja na Allaah kwa yule mnyama wa kwanza na wanyama wengine hawatajiwi jina la Allaah.

Ibn Baaz: Anachinja kwa mkono wake au ni mashine ndio inachinja?

Mwanafunzi: Anachinja kwa mkono wake kwa kutumia mashine. Kwa maana nyingine mashine inazunguka na kila inapopita anachinja kwa mkono wake.

Ibn Baaz: Inatosha akitaja jina la Allaah juu ya wanyama wote. Akitaja jina la Allaah kwa yule mnyama wa kwanza na anawakusudia wote inatosha – Allaah akitaka, kwa sababu wanakufa wote mara moja.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24015/هل-تكفي-التسمية-لعدة-ذباىح-على-الاولى-منها
  • Imechapishwa: 17/08/2024