Ameyarudia maasi baada ya kuapa kuyaacha

Swali: Mtu anaapa kuacha maasi kisha baadaye anayarudilia?

Jibu: Ni lazima kwake kutoa kafara na tawbah yote mawili. Akiapa kwamba hatovuta sigara wala hatokunywa pombe basi atalazimika kutekeleza kiapo chake, kwa sababu hiyo ni haki. Analazimika kujizuilia na maasi hata kama hakuapa. Anawajibika kujizuilia na maasi hata kama hakuapa. Lakini akiapa amejitilia mkazo msimamo na hivyo wajibu kwake unakuwa mkubwa zaidi. Hata hivyo ikitokea akavunja kiapo na hivyo anavuta sigara na kunywa pombe, basi atalazimika kutubia pamoja na kutoa kafara ya kuvunja kiapo chake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24017/حكم-من-يحلف-على-ترك-المعصية-ثم-يعود
  • Imechapishwa: 17/08/2024