Ibn Baaz kuhusu kuyatembelea makaburi siku ya ijumaa

Swali: Ni ipi hukumu ya kuyatembelea makaburi kufanya maalum siku ya ijumaa?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na msingi. Lililowekwa katika Shari´ah ni yule mwenye kuyatembelea makaburi ayatembelee wakati wowote itapokuwa sahali. Ni mamoja ikawa usiku au mchana. Kuhusu kuyatembelea siku maalum au usiku maalum ni Bid´ah isiyokuwa na msingi wowote. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atayezusha katika amri yetu hii yasiyokuwemo yatarudishwa.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

“Atakayefanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu kitarudishwa.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.binbaz.org.sa/fatawa/2718
  • Imechapishwa: 15/10/2016