Ibn ´Uthaymiyn kuyatembelea makaburi siku ya ´Iyd na ijumaa

Swali: Ni ipi hukumu ya kutembelea makaburi mtu akafanya maalum siku ya ´Iyd mbili na siku ya ijumaa? Ndani ya masiku hayo wanatembelewa wale wapendwa tu au maiti wote kwa jumla?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na msingi. Kuyatembelea makaburi kufanya maalum siku ya ´Iyd na kuamini ya kwamba jambo hilo limewekwa katika Shari´ah inazingatiwa kuwa ni Bid´ah kwa kuwa haikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala hayakusemwa na mwanachuoni yeyote.

Kuhusu kuyatembelea siku ya ijumaa yamesemwa na baadhi ya wanachuoni ya kwamba matembezi yanatakiwa kuwa siku ya ijumaa. Pamoja na hivyo hawakutaja upokezi wowote juu ya hilo kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa’iz, uk. 70
  • Imechapishwa: 15/10/2016