Swali: Kwetu chuo kikuu wapo Raafidhwah wengi. Je, nianze kuwatolea salamu?
Jibu: Ikiwa unawajua kuwa ni Raafidhwah wanaodhihirisha Bid´ah zao, basi usianze kuwatolea wala kuwaitikia salamu. Wanatakiwa kususwa. Ama ikiwa hawakudhihirisha na kinyume chake wamezificha, katika hali hiyo wanatolewa salamu.
Swali: Hawaswali msikitini?
Jibu: Hawaswali pamoja na mkusanyiko. Hii ni miongoni mwa Bid´ah.
Swali: Kwa maana wasiitikiwe?
Jibu: Wala wasianze kutolewa salamu mpaka waswali pamoja na waislamu, mpaka wainusuru Sunnah na wajiepushe mbali na Bid´ah.
Swali: Vipi kuhusu Suufiyyah waliochupa mipaka?
Jibu: Suufiyyah ikiwa wataidhihirisha Bid´ah yao. Vinginevyo wanatakiwa kutolewa salamu. Ikiwa wataidhihirisha Bid´ah ya ukafiri au ile inayolazimisha kuwakata, katika hali hiyo hawatolewi salamu. Na ikiwa hawakudhihirisha kitu chochote, wako pamoja na waislamu katika swalah na katika matendo yao, katika hali hiyo watolewe salamu. Huna la kuzingatia isipokuwa yanayoonekana waziwazi kwa nje.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28502/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D8%A8%D8%AA%D8%AF%D8%A7%D8%A1-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%A7%D9%81%D8%B6%D8%A9-%D9%88%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%A8%D8%AA%D8%AF%D8%B9%D8%A9%C2%A0%D8%A8%D8%A7%D9%84%D8%B3%D9%84%D8%A7%D9%85
- Imechapishwa: 20/04/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)