Ibn Baaz kuhusu kutundika Aayah za Qur-aan kwenye majumba na misikiti

Swali: Ni ipi hukumu ya kutundika baadhi ya Aayah za Qur-aan au Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) zilizoko kwenye vibao ndani ya majumba?

Jibu: Ninavyoona ni kwamba kufanya hivi haijuzu kwa kuwa ni kuitia mitihanini Qur-aan na kwa sababu Qur-aan haikuteremshwa ili itundikwe kwenye kuta za Msikitini au majumbani. Imeteremshwa ili itendewe kazi na ihifadhiwe. Hili ndio lengo la kuteremshwa. Hivyo isitundikwe kwenye kuta za Misikitini au mfano wake. Inachotakiwa ni kutofanya hivyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=6906
  • Imechapishwa: 05/05/2015