Ibn Baaz kuhusu kuswali Sunnah Rak´ah nne kwa Tasliym moja

Swali: Je, kuna uthibitisho sahihi kuhusu swalah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuswali Rak´ah nne kabla ya Dhuhr bila kutoa salamu? Hadiyth isemayo:

”Swalah ya usiku na mchana ni [Rak´ah] mbilimbili.”?

ni Swahiyh? Vipi zinaoanishwa?

Jibu: Swalah ya kuswali Rak´ah nne mfululizo bila kutoa salamu ina udhaifu. Haikuthibiti kutokana na ninavyojua. Sunnah ni yeye kuswali kila baada ya Rak´ah mbili:

”Swalah ya usiku na mchana ni [Rak´ah] mbilimbili.”?

Hadiyth hii ni Swahiyh. Imekuja katika Hadiyth Swahiyh ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

”Swalah ya usiku na mchana ni [Rak´ah] mbilimbili.”

Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah zake za sunnah akitoa salamu kila baada ya Rak´ah mbili. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza:

“Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiswali usiku Rak´ah kumi na akitoa salamu kila baada ya Rak´ah mbili kisha alikuwa akihitimisha kwa Rak´ah moja ya Witr.”

Hata hivyo inajuzu kuunganisha Rak´ah kwa Witr, kama vile kuswali Rak´ah tano mfululizo, tatu au saba bila kutoa salamu katikati, kama ilivyopokelewa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini haifai kwa mtu kuswali swalah ya kujitolea Rak´ah nne au sita au nane mfululizo bila kutoa salamu kila baada ya Rak´ah mbili. Kufanya hivyo ni kwenda kinyume na sunnah. Sunnah ni kutoa salamu baada ya kila Rak´ah mbili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25133/هل-صح-صلاة-النبي-اربعا-قبل-الظهر-دون-فصل
  • Imechapishwa: 05/02/2025