Ibn Baaz kuhusu kurekodi kwa video camera mihadhara ya dini

Swali: Ni ipi hukumu ya kurekodi mihadhara kwa kifaa cha video camera ili maeneo mengine yaweze kufaidika nao na faida ienee zaidi?

Jibu: Hili ni jambo linalohitaji kutazamwa vizuri. Kurekodi katika kanda ni jambo linalotakikana na hakuna haja ya kuchukua picha. Lakini nyakati fulani picha inaweza kuhitajika ili mtu awe na uhakika kuwa mzungumza ni mtu fulani. Kwa sababu picha inaweka wazi yule mzungumzaji. Kuna vilevile kuwepo sababu nyinginezo.

Mimi nimechukua msimamo wa kunyamaza juu ya jambo hili. Nimefanya hivo kutokana na zile Hadiyh zilizopokelewa kuhusu kuchukua picha viumbe vyenye roho na matishio makali ya adhabu juu ya hilo. Ingawa wako ndugu zetu katika wanachuoni ambao wameona hakuna neno kufanya hivo kutokana na yale manufaa yenye kuenea. Lakini hata hivyo mimi katika jambo hili nimechukua msimamo wa kusimama kutokana na ile khatari kubwa ya picha. Jengine ni kutokana na zile Hadiyth zilizothibiti kwa al-Bukhaariy, Muslim na vitabu vyenginevo zinazobainisha kwamba watu wataokuwa na adhabu kali siku ya Qiyaamah ni wale watengeneza picha na pia Hadiyth zinazowalaani watengeneza picha. Zipo Hadiyth nyenginezo vilevile.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (05/355)
  • Imechapishwa: 26/06/2020