Swali: Je, ipo tofauti katika kutangamana na wazushi ambaye amezusha kwa sababu ya kuelewa kimakosa na mzushi ambaye amezusha kwa sababu ya kufuata matamanio yake?

Jibu: Pasi na kujali mzushi amezusha kwa sababu ya kufahamu kimakosa na akadhani kuwa alivyoelewa ndio haki au hakuelewa kimakosa bali yeye anafuata tu kibubusa, ni lazima mtu amtambulishe mfasiri huyu kuwa amekosea. Akishatambulishwa kosa lake na akakataa kujirejea, basi atazingatiwa kuwa ni mwenye kunga´ng´ania Bid´ah yake. Kwa ajili hiyo itatakiwa kumkata ili ajirudi katika Bid´ah yake.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath-ur-Rahiym al-Waduud, uk. 254
  • Imechapishwa: 26/06/2020