Ibn Baaz kuhusu Jamaa´ah ya pili msikitini

Swali: Ni ipi hukumu ya Jamaa´ah inayochelewa kukaswaliwa Jamaa´ah nyingine baada ya Swalah ya Jamaa´ah iliyoadhiniwa pamoja na Imamu mteuliwa?

Jibu: Hakuna neno. Wakikuta Imamu ameshaswali, waswali Jamaa´ah nyingine na waswali kama jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyoswali Jamaa´ah nyingine kwa mtu ambaye aliingia na akakuta Swalah imeshampita, akawaambia baadhi ya waliokuwepo pale “Ni nani ambaye atamtolea Swadaqah na kuswali naye Jamaa´ah?” Kwa kuwa Swalah ya watu wawili sio sawa na Swalah ya mtu mmoja. Jamaa´ah ya kwanza ikimpita na akakutana na watu wengine, waswali pamoja Jamaa´ah. Hili limefanya Anas na Maswahabah wengine (Radhiya Allaahu ´anhum).

Ama kauli ya wanachuoni wanaosema kuwa haitakiwi kuswali Jamaa´ah [mbali na ile Jamaa´ah ya kwanza], wanachotakiwa ni kurudi majumbani mwao na kuswali, hii si lolote. Ni kauli isiyokuwa na nguvu na ni dhaifu. Inaenda kinyume na Sunnah na kanuni za Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=6898
  • Imechapishwa: 04/12/2014