Swali: Nikiwa niko na ndugu ambao haswali na wanafanya maovu nyumbani, mchanganyiko na mengineyo, na siwezi kuwakataza. Je, itakuwa ni wajibu kwangu kuwatembelea?

Jibu: Ikiwa ndugu zako wanafanya mambo ya maovu, ima uunge kizazi nao kwa ajili ya kuwakataza na kuwapa nasaha. Hili ni jambo zuri kwako ukawatembelea kwa ajili ya kuwakataza na kuwanasihi. Wakipokea nasaha, himdi zote ni za Allaah, wakiendelea na batili yao wakate na usiwatembelee kwa kuwa hawastahiki kutembelewa maadamu wanafanya maovu ya wazi wazi kama ya kunywa pombe, kuacha swalah na mfano wa madhambi kama hayo ya wazi. Kuacha swalah ni ukafiri. Ni dhambi kubwa kuliko madhambi makubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=6899
  • Imechapishwa: 04/12/2014