Ibn Baaz kuhusu filamu za kuwaigiza Mitume, Maswahabah na wanachuoni

Swali: Ni upi mtazamo wako kuhusu barnamiji za Televisheni ambapo wanaweka tamthili [filamu] za kidini ndani yake wanawaigiza Maswahabah na Taabi´uun na wanachuoni?

Jibu: Hili limeshatangulia zaidi ya mara moja ya kwamba kuwaigiza Maswahabah na Mitume ni jambo lisilojuzu. Hili limefanyiwa utafiti na kamati ya wanachuoni wakubwa na kufikia kuonelea kuwa haijuzu kuwaigiza Maswahabah na Mitume sehemu yoyote. Kwa kuwa jambo hili linapelekea katika madhara mengi. Linaweza kupelekea kuwasemea uongo, mfumo usiokuwa mzuri na usiostahiki, kuwafanyia mzaha na maskhara. Jambo hili halijuzu, sawa ikiwa ni kwa Mitume au Maswahabah.

Ama wasiokuwa Mitume na Maswahabah hili linahitajia kuangaliwa. Inaweza kuwa inajuzu [ikiwa ni kwa sauti tu pasina njia ya picha] na inaweza kuwa haijuzu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=6902f
  • Imechapishwa: 04/12/2014