Ibn Baaz kuhusu Basmalah kabla ya wudhuu´

Swali: Hadiyth zinazosema mtu anatakiwa kusema ”Bismillaah” kabla ya kuanza kutawadha njia zake zote ni dhaifu.

Jibu: Baadhi yao wameona kuwa ni nzuri. Kwa msemo mwingine ni kwa minajili ya nzuri kutokana na nyenginezo. Mfano wa wanazuoni hao ni Ibn-us-Swalaah na Ibn Kathiyr  (Rahimahu Allaah) katika kitabu chake cha ”at-Tafsiyr” ambaye amesema kuwa ni nzuri na katika tafsiri ya Suurah ”al-Maaidah”.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25156/ما-صحة-حديث-البسملة-في-الوضوء
  • Imechapishwa: 08/02/2025