Hajj na ´Umrah kwa niaba ya wafu na waliohai

Swali: Vipi kuhusu yule anayefanya ´Umrah kwa niaba ya baba au mama yake?

Jibu: Hapana neno ikiwa wameshafariki au ikiwa hawawezi kwa sababu ni wazee sana au wagonjwa wasioweza kupona. Hali hii ni kama mfu au mgonjwa asiyeweza kupona au mzee sana. Kuna mwanamke alimjia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema:

“Ee Mtume wa Allaah, baba yangu ni mzee mkubwa hawezi kukaa imara juu ya mnyama wa safari. Je, nimhijie?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Hiji kwa niaba ya baba yako.”

Mtu mwingine alimwendea na kusema: “Ee Mtume wa Allaah, baba yangu ni mzee mkubwa hawezi kuhiji wala kusafiri. Je, nimhijie na kufanyia ´Umrah?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Hiji kwa niaba ya baba yako na fanya ´Umrah.

Swali: ´Umrah ni ´ibaadah ya Sunnah?

Jibu: Ni ´ibaadah ya Sunnah kwa mfu na asiyeweza, ni mamoja iwe ni Sunnah au ni ya faradhi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25155/ما-حكم-الحج-والعمرة-عن-الوالدين-احياء-وامواتا
  • Imechapishwa: 08/02/2025