Swali: Vipi kuhusu mtu ambaye amekusudia kuacha baadhi ya siku za funga na swalah lakini baadaye akatubia?
Jibu: Tawbah inatosha. Akitubia basi Allaah anamsamehe. Ikiwa aliacha kuswali, akafanya aina ya ukafiri au kichenguzi aina moja wapo cha Uislamu, basi tawbah inatosha. Akitubia Allaah anamkubalia tawbah yake na wala hahitaji kulipa. Hata hivyo swawm anatakiwa kuilipa. Hukumu ni moja ikiwa alichelewesha kuhiji anapaswa kuhiji na wala hakufuru. Lakini kuhusu kuacha kuswali ni ukafiri kwa mujibu wa maoni sahihi hata kama hakupinga uwajibu wake. Akiacha kuswali kisha baadaye Allaah akamwongoza basi hahitaji kulipa, inamtosha kutubia.
Swali: Unakusudia kuwa swawm na swalah vinalingana?
Jibu: Hapana, havilingani. Kuacha swalah ni ukafiri. Mwenye kufa katika hali hiyo amekufa hali ya kuwa ni kafiri. Akisilimu na akatubia kwa Allaah halazimiki kulipa. Lakini ikiwa anaswali na ni mtu mwema, hata hivyo akaacha baadhi ya siku za swawm, huyu ndiye anayepaswa kulipa pamoja na kutubia. Kuacha kufunga sio ukafiri mkubwa, hapana. Baadhi ya Salaf wamesema kuwa anakufuru. Lakini maoni sahihi ni kwamba hakufuru kwa kitendo hicho, bali anakuwa mtenda dhambi. Anayekula kwa makusudi anakuwa mtenda madhambi na wala hakufuru. Hata hivyo analazimika kulipa na kutubia. Swalah ni kubwa zaidi.
Swali: Vipi ikiwa hafungi wala kuswali katika wakati mmoja?h
Jibu: Ikiwa haswali na wala hafungi halazimiki kulipa swawm wala swalah, badala yake anapaswa kutubia. Kwa sababu alikuwa mwenye kuritadi na mwenye kuritadi halipi. Lakini ikiwa anaswali na akaacha baadhi ya siku za swawm, anatakiwa kulipa swawm hizo.
Swali: Vipi ikiwa anaacha baadhi ya swalah tu?
Jibu: Kuacha baadhi ya swalah ni ukafiri. Akiacha baadhi ya swalah kwa namna ya kwamba mara anaswali na mara nyingine haswali, huyu anakuwa kafiri.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24474/ما-حكم-قضاء-الصلاة-والصوم-لمن-تاب
- Imechapishwa: 23/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)