Ibn Baaz akijibu maswali kadhaa muhimu kwa anayetoa harufu mbaya kuja kuswali msikitini

Swali: Je, ambaye amekula kitunguu saumu anaruhusiwa kuacha swalah ya mkusanyiko?

Jibu: Ni haramu kwake akila kwa sababu ya kuacha mkusanyiko. Hata hivyo hapana vibaya akila kwa sababu anahitaji au kwa lengo la matibabu.

Swali: Vipi ikiwa ndio mazowea yake?

Jibu: Asile ilihali kunamzuia kuswali na kunawakera watu, kwa sababu kufanya hivo kunaweza kuwa ni ujasiri wa kipumbavu wa kukosa swalah ya mkusanyiko.

Swali: Ijapo atakuwa nchi kavu?

Jibu: Asiswali pamoja nao, aswali peke yake.

Swali: Vipi wakikubaliana wote?

Jibu: Hapo wataswali wote, kwa sababu kila mmoja atakuwa na ugonjwa [huo wa kutoa harufu].

Swali: Lakini (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… asiukurubie msikiti wetu.”[1]

Vipi ikiwa watakuwa nchi kavu kwenye hema na hawana msikiti?

Jibu: Lakini atawaudhi marafiki zake.

Swali: Si imepokelewa pia kuwa Malaika wanaudhika?

Jibu: Asikurubie msikiti hata kama hakuna mtu, kwa sababu Malaika wanaudhika kwa yale yanayowaudhi watu.

Swali: Je, hilo linahusu pia sigara?

Jibu: Ni kila ambacho kina harufu mbaya.

Swali: Katika Hadiyth kumetajwa kitunguu saumu na kitunguu maji. Katika kichwa cha khabari cha mlango kumetajwa: “Mlango unaozungumzia kitunguu saumu, kitunguu maji na figili.”?

Jibu: Ni mfano wake. Maana ni moja.

Swali: Bora ni yeye asubiri mpaka iondoke ile harufu kwa sababu asiwakere Malaika au aswali papohapo?

Jibu: Aswali nyumbani kwake.

Swali: Je, nyumbani kwake asubiri mpaka iondoke ile harufu?

Jibu: Hapana, apunguze ile harufu na aswali nyumbani kwake.

Swali: Vipi kuhusu ambao wametofautisha na kusema kwamba ikiwa harufu ni yenye kuenea msikiti mzima ndio mtu ambaye amekatazwa, lakini ikiwa harufu imekomeka kwake pekee…

Jibu: Hapana, harufu inamkera na inawakera walio pembeni yake. Sio lazima harufu isambae msikiti mzima… harufu inamuudhi jirani yake aliyeko kuliani na kushotoni.

Swali: Je, makusudio ni kukatazwa ile swalah inayoswaliwa sasa?

Jibu: Ni mamoja ile swalah inayoswaliwa sasa au nyenginezo muda wa kuwa bado yuko na harufu ya kitunguu saumu na kitunguu maji.

Swali: Ikiwa harufu itaendelea kwa vipindi vitano vya swalah au vipindi sita vya swalah?

Jibu: Asisogelee msikiti ijapo ni swalah za faradhi tano au sita.

Swali: Je, inamuhusu pia ambaye ana harufu mbaya ya mdomo au kikwapa?

Jibu: Ajitibishe na kutumia dawa. Ikiwa ni maradhi ajitibishe.

Swali: Makatazo ni kwa njia ya uharamu?

Jibu: Huo ndio udhahiri wa Hadiyth kwamba ni haramu.

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb”, nr. 333))

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23790/حكم-المسجد-والجماعة-لمن-به-راىحة-كريهة
  • Imechapishwa: 01/05/2024