Ibn Baaz akijibu maswali kadhaa kuhusu josho la siku ya ijumaa

Swali: Vipi kuhusu josho la ijumaa?

Jibu: Ni Sunnah iliyokokotezwa.

Swali: Atawadhe au aoge tena yule ambaye ameoga kwa ajili ya ijumaa baada ya Fajr kisha akapatwa na hadathi?

Jibu: Inatosha kutawadha. Siku ya ijumaa yote, nikikusudia kabla ya kuswali, ni wakati wa kuoga. Hata hivyo bora ni kuoga wakati mtu anataka kwenda kuswali.

Swali: Vipi kwa ambaye anaoga baada ya Fajr?

Jibu: Inatosha baada ya Fajr. Lakini bora ni kuoga pale ambapo anataka kwenda kuswali ijumaa. Mtu aoga pindi anapotaka kwenda. Bora ikiwa inawezekana ni yeye kuoga wakati anapotaka kwenda kuswali ijumaa.

Swali: Vipi akioga baada ya Fajr kisha akalala?

Jibu: Haijalishi kitu. Lengo limefikiwa muda wa kuwa ameswali baada ya Fajr. Hata hivyo bora ni kuoga wakati mtu anataka kwenda kuswali.

Swali: Je, inafaa kwake kuoga kabla ya Fajr?

Jibu: Hapana, ndani ya siku. Josho linakuwa siku ya ijumaa. Josho linakuwa wakati wa mchana.

Swali: Josho baina ya adhaana na Iqaamah?

Jibu: Inasihi maadamu ni baada ya Subh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23797/ما-حكم-غسل-الجمعة-ووقته
  • Imechapishwa: 02/05/2024