Kubadilisha maeneo kwa ambaye anaswali swalah nyingi za Sunnah

Swali: Ikiwa mtu anaswali swalah nyingi zinazopendeza na baada ya kila Tasliym anabadilisha maeneo?

Jibu: Halina msingi.

Swali: Hadiyth ya al-Mughiyrah bin Shu´bah:

“Je, anashindwa yeyote katika nyinyi anapomaliza kuswali akasogea mbele au akarudi nyuma au akaenda kuliani au kushotoni?”

Jibu: Ni dhaifu.

Mwanafunzi: Viipi kitendo cha Ibn ´Umar?

Jibu: Hilo ni katika Ijtihaad yake.

Swali: Wako ambao wanajengea hoja kitendo hicho kwamba Siku ambayo ardhi itaelezea khabari zake ya kwamba ni kule mtu kuswali maeneo mbalimbali?

Jibu: Hapana, haina msingi. Aswali mahali pake. ´Ibaadah hazitokamani kwa khiyari au maoni ya mtu. ´Ibaadah ni kwa mujibu wa dalili.

Swali: Kwa hivyo bora mtu anapomaliza kuswali faradhi aswali mahali pake palepale?

Jibu: Mahali pake. Vinginevyo bora zaidi aenda kuswali nyumbani kwake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23789/حكم-الانتقال-من-مكان-لاخر-في-صلاة-النافلة
  • Imechapishwa: 01/05/2024