Ibaadhiyyah wanawachukuliaje waislamu waliokufa katika madhambi makubwa?

04- Wanapinga uombezi na kwamba waislamu watenda madhambi watadumishwa Motoni milele

Masuala haya ni miongoni vilevile mwa mambo ambayo Ibaadhiyyah wamewafuata viongozi wao Mu´tazilah. Hoja zao katika hilo hazina mashiko. Ahl-us-Sunnah wameraddi upotevu wao huu kwa yale yaliyotajwa katika Qur-aan na Sunnah. Imaam al-Aajurriy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tambua – Allaah akurehemu – ya kwamba wale wanaopinga uombezi wanadai ya kwamba yule atakayeingia Motoni hatotoka humo. Wanasema uongo kwa madhehebu haya Mu´tazilah… “

Mpaka alipofikia kusema:

“Huu sio mwenendo wa waislamu. Bali huu ni mwenendo wa wale waliopotea kutokamana na njia ya haki na shaytwaan akacheza nao.”

Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Yule mwenye kukadhibisha uombezi basi hana fungu nao.”

  • Mhusika: Shaykh ´Abdullaah as-Salafiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ibaadhwiyyah fiy miyzaan Ahl-is-Sunnah, uk.19
  • Imechapishwa: 11/02/2017