Swali: Je, mtu anapata ujira wa kumfadhili yatima ikiwa mtu huyo analazimika kumhudumia?

Jibu: Yatima ni yule ambaye amemkosa baba yake akiwa bado ni mtoto. Huyu ndiye yatima. Yanatakiwa yatimie masharti mawili:

1 – Amemkosa baba yake.

2 – Awe bado hajabaleghe.

Huyu ndiye anaitwa yatima. Mtoto huyu anatakiwa kutendewa wema akiwa ni fakiri. Akiwa sio fakiri basi hawahitajii watu na anachokuwa anahitajia ni yale malezi kwa mujibu wa dini peke yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21629/هل-يحصل-اجر-كفالة-اليتيم-لمن-تجب-نفقتهم
  • Imechapishwa: 30/08/2022