Huyu ndiye mgonjwa anayetakiwa kulisha chakula badala ya swawm

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anaacha kufunga kwa sababu ya maradhi sugu yanayomwandama sasa kwa miaka kadhaa?

Jibu: Madaktari wakithibitisha kuwa magonjwa yake hayatarajiwi kupona, ingawa Allaah ndiye mponyaji. Wakati mwingine madaktari wanathibitisha kuwa hatopona lakini baadaye akaponywa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Muhimu ni kwamba madaktari wakithibitisha kuwa magonjwa yake hayatarajiwi kupona, basi ni sawa akalisha chakula masikini kwa kila siku moja itayompita. Mola wetu (´Azza wa Jall) amesema:

وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ

”Kwa wale wanaoiweza lakini kwa tabu watoe fidia.”[1]

Hivo ndivo alivyokuwa akifanya Maalik wakati alipokuwa na umri wa kutoweza kufunga akawa analisha chakula masikini kwa kila siku moja iliyompita.

[1] 02:184

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 78
  • Imechapishwa: 17/03/2024