Hukumu ya swalah ambayo mtu anasoma at-Tahiyyaat nusu

Swali: Kuna mwanamke ni mtumzima sana na anaswali. Lakini hata hivyo anasema kuwa hajui zaidi ya kusema “at-Tahiyyaatu lillaahi, was-Swalawaatu wat-Twayyibaat” tu. Ni ipi hukumu ya hilo na Swalah yake inasihi au hapana?

Jibu: Ikiwa hajui at-Tahiyyaat isipokuwa maneno haya mane:

التحيات لله، و الصلوات و الطيبات

“Maadhimisho, swalah na mazuri yote yanamstahikia Allaah.”

yale yaliyomshinda yanamkatikia [hayamuwajibikii]. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake.” (02:286)

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Basi mcheni Allaah muwezavyo” (64:16)

Hatujui badala ya at-Tahiyyaat.

Kuhusu al-Faatihah mtu ikimshinda tunamwambia asome kitu kingine katika Qur-aan kwa kadiri ya al-Faatihah. Ikiwa hajui kitu chochote katika Qur-aan tunamwambia alete Tasbiyh, Tahliyl na Takbiyr kwa kiasi cha al-Faatihah kisha arukuu. Ama kuhusu Tashahhud haina badala. Ikiwa hajui jengine zaidi ya haya maneno mane itakuwa imemkatikia kutokana na maneno Yake (Ta´ala):

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Basi mcheni Allaah muwezavyo” (64:16)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 07
  • Imechapishwa: 23/09/2020