Mzazi hataki mwanae aoe kwa hoja ya umasikini

Swali: Mimi ni kijana ninataka kuoa na nina mama yangu amekataa. Udhuru wake ni kwamba sisi bado tuko katika nyumba ya kupanga na kwamba yeye yuko na baadhi ya madeni. Je, inajuzu kwangu kwenda kinyume na ridhaa yake kwa kuwa mimi nina haja ya kuoa na badala yake niweke mtu aniposee kwa kuwa yeye amekataa kuniposea? Ninaomba nasaha kwangu na kwake. Nini anachofanya mtu ambaye hali yake ni kama hii yangu? Mimi ni mfanya kazi na ninaweza kukusanya mahari au nikachukua huku na kule.

Jibu: Kwanza haijuzu kwa mama kuingilia kati ya mtoto na kuoa. Asimkataze. Wajibu kwake ni yeye kumnasihi mtoto wake kama jinsi anavyojinasihi yeye mwenyewe na amsaidie katika kumtii Allaah na katika yale yanayomfaa. Bila ya shaka kuoa ni katika kumtii Allaah na ni katika mambo yanayomfaa. Haimdhuru kitu akioa, bali kinyume chake anazidiwa na kheri. Kwa kuwa pengine akaoa mwanamke mwema ambaye atakuwa anamhudumia yeye na mama yake, kama jinsi hilo linavyotokea mara nyingi.

Kuhusiana na yeye, nasema kwamba ni sawa kwako kuoa ingawa mama yako atachukia. Kwa kuwa haya ni maslahi kwako na kuzuia madhara kwako na hili halimdhuru mama kitu. Wewe hivi sasa tafuta mwanamke mwema na uoe. Ninavyofikiria ni kwamba mama atapoona mambo yanasonga mbele ataridhia [mwishoni].

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 01
  • Imechapishwa: 23/09/2020