Hukumu ya kuweka alama kwa ajili ya kunyoosha safu

Swali: Kufunga kamba misikitini kwa sababu ya kunyoosha safu ni katika Sunnah?

Jibu: Sijui juu ya jambo hili msingi unaojulisha kuwa ni katika Sunnah kama ambavo sijui kwa mujibu wa Shari´ah jambo linalofahamisha kulikataza. Kwa sababu tumeamrishwa kuzinyoosha safu na kutozipindisha. Baadhi ya watu wakichukua kitu kinachosaidia kunyoosha safu, kutokuwa mbele wala nyuma basi nataraji kuwa hakuna neno kufanya hivo. Lakini kusema kuwa ni Sunnah sijui jambo hilo.

Sunnah ni kule kutilia bidii kunyoosha safu, kuamrisha kuinyoosha na kuamrisha baadhi wasiwe mbele juu ya wengine. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaamrisha kufanya hivo kabla ya kuanza swalah. Alikuwa akiwaamrish na akitilia bidii jambo hilo mpaka safu inyooke. Sijui kama kuna ubaya wowote ikiwa baadhi ya watu wataweka kamba kwa kiwango cha safu ili safu iweze kunyooka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4550/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D8%AA%D8%AE%D8%A7%D8%B0-%D8%B9%D9%84%D8%A7%D9%85%D8%A7%D8%AA-%D8%A8%D8%B5%D9%81%D9%88%D9%81-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D9%84%D8%AA%D8%B3%D9%88%D9%8A%D8%AA%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 14/10/2020