Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa nguo ya rangi nyekundu tupu?
Jibu: Baadhi ya wanazuoni wameona kuwa inachukiza kuvaa nguo ya rangi nyekundu tupu isiyokuwa na mchanganyiko mwengine. Wengine hawakuchukizwa na jambo hilo kutokana na kusimuliwa kwa Hadiyth nyenginezo zinazotamka kwa kuachia kuvaa mavazi mekundu na meusi.
Swali: Ni yepi maoni sahihi?
Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi. Kinachodhihirika ni kwamba inajuzu kuvaa nguo nyekundu. Hilo ndio sahihi zaidi. Hadiyth zilizopokelewa kuhusu kuvaa nguo nyekundu ni Swahiyh na zimethibiti zaidi.
Swali: Vipi ikiwa vazi hilo jekundu ni la umashuhuri?
Jibu: Haijuzu kuvaa vazi la umashuhuri; ni mamoja jekundu, kijani kibichi, jeusi wala jeupe.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23284/ما-حكم-لبس-الاحمر-الخالص
- Imechapishwa: 20/12/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
Bibi harusi kuvaa gauni jeupe siku ya harusi
Swali: Ni ipi hukumu kwa bibi harusi akivaa mavazi meupe usiku wa harusi? Jibu: Hakuna neno katika hilo kwa sababu kila tukio lina vazi lake, isipokuwa ikiwa itakuwa na maana ya kuwaiga makafiri au wanawake waasi, kwa kuwa hili ni jambo jingine sawa ikiwa ni nguo nyeupe, nyekundu au nyeusi. Ama…
In "Jumla kuhusiana na vazi la mwanamke"
Ibn ´Uthaymiyb kuhusu Hijaab nyeupe, kijani au nyekundu
Swali: Inajuzu kwa mwanamke kuvaa Hijaab nyeupe, kijani au rangi nyenginezo ikiwa hii ndio desturi kwa watu wake na khaswa ikiwa baadhi ya wanawake wajinga wanamuona ni kituko pindi anapovaa Jilbaab nyeusi? Jibu: Hakuna neno ikiwa hii ni desturi ya nchi akavaa vazi leupe. Lakini hata hivyo isiwe katika shakili…
In "Mwanamke kujifananisha na wanaume na kinyume chake"
43. Baadhi ya hukumu zinazomuhumu mwanamke katika Hajj na ´Umrah IX
7 - Inajuzu kwa mwanamke katika hali ya Ihraam yake kuvaa nguo za wanawake anazotaka zisizokuwa na mapambo, hazifanani na nguo za wanaume, si zenye kubana kuonyesha fomu ya viungo vyake, si nyepesi zenye kuonyesha kilicho nyuma yake na si fupi zenye kuishilia kwenye miguu yake au mikononi mwake. Bali…
In "08. Sura ya nane: Hukumu zinazomuhusu mwanamke katika Hajj na ´Umrah"