Swali: Baadhi ya watu wamezowea katika msikiti Mtakatifu wa Makkah anapoadhini muadhini adhaana ya pili basi utaona watu wengi wanasimama kuswali Rak´ah mbili.

Jibu: Hapana, ni kwenda kinyume na Sunnah. Sunnah ni kuketi chini na kunyamaza. Hali hii haihusiani na kuswali baina ya kila adhaana na Iqaamah.

Swali: Vipi ikiwa ni wakati wa ile adhaana ya kwanza?

Jibu: Haina msingi. Adhaana ya kwanza ni kwa ajili tu ya kuzindua. Baada ya adhaana ya kwanza hakuna swalah. Bora ni kuacha kufanya hivo. Hukumu hiyohiyo inahusiana na baada ya adhaana ya kwanza. Wanatakiwa wajiandae kunyamaza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23810/حكم-صلاة-ركعتين-بعد-الاذان-الثاني-للجمعة
  • Imechapishwa: 14/05/2024