Hukumu ya kuitwa “Hakimu wa mahakimu”

Swali: Vipi kuitwa ´qaadhi wa maaqadhi`?

Jibu: Haitakikani kufanya hivo, kwa sababu maana yake ni hakimu wa mahakimu. Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) ameweka mlango kichwa cha khabari “qaadhi wa maqaadhi” na mfano wake[1]. Alichokusudia ni kubainisha ya kwamba haifai, kwa sababu hakimu wa mahakimu inakaribia kuwa na maana ya mtawala wa watawala. Kwa hivyo haitakikani. Lakini kusema qaadhi wa maqaadhi wa nchi fulani kuna wepesi fulani. Kusema qaadhi wa maqaadhi wa Dameski, Misri au ar-Riyaadh kuna wepesi kidogo kwa sababu kumefungamanishwa. Bora kuliko hivo ni kusema raisi  wao au mkuu wao.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/46-kuitwa-qaadhi-wa-maqaadhi-na-mfano-wake/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24218/هل-يجوز-التسمي-بقاضي-القضاة
  • Imechapishwa: 14/09/2024