Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa ´Abaa´ah zenye mikono mipana pamoja na kuzingatia kwamba zinakuwa ni zenye kufunika mikono na si zenye marangi?

Jibu: Kile ninachoona kuwa ni kwamba wanawake wetu wanatakiwa kuwa na utu wa Kiislamu na wabaki katika ´Abaa´ah zilizozoeleka ambazo zinakuwa juu ya kichwa. Kwa sababu zinasitiri bora zaidi. ´Abaa´ah zinazowekwa juu ya mabega zinaonyesha mabega na zinaonyesha urefu na ufupi wa shingo. Jengine ni kwamba ni sababu ya kwenda mbali zaidi. Tunachomaanisha ni kwamba wanawake hawatosimama hapo tu midhali wamefunguliwa mlango. Mimi naona kuwa mwanamke abaki katika vazi lake la mwanzo linalowekwa juu ya kichwa chake na kushuka kwenye mwili wake mzima.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1727
  • Imechapishwa: 04/05/2020