Swali: Siku hizi kumekithiri maongezi katika magazeti na TV na Khutbah za Ijumaa kwenye misikiti kuhusu historia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na haki zake na tabia yake kwa sababu mazao yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yamekaribia. Ni ipi hukumu ya kitendo hichi na ni ipi nasaha yako kwa Ummah juu ya hilo?
Jibu: Ndio, kuzungumzia historia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), tabia yake, kukumbusha juu ya kumpenda na kumfuata ni jambo limewekwa katika Shari´ah. Lakini hata hivyo haitakiwi kulikhusisha na wakati fulani. Hili linafanywa wakati wote katika mwaka.
Kuhusiana na yule mwenye kukhusisha wakati huu na hazungumzii historia na sifa za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa katika wakati huu, hii ni njia inayopelekea katika kuhuisha Bid´ah. Zindukeni juu ya hilo. Kukhusisha wakati huu ambapo ni karibu na kipindi cha Bid´ah, hii maana yake ni kushirikiana na watu wa Bid´ah katika kuhuisha Bid´ah.
Hakuna kitu kimechokufanya kukumbushia historia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati huu isipokuwa ni kwa sababu kunataka kuhuishwa Bid´ah hii karibuni. Huyu anakuwa ni mwenye kushirikiana nao na kuwapa nguvu.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (10) http://alfawzan.af.org.sa/node/2125
- Imechapishwa: 05/07/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)