Huhitajii vitabu vya Sayyid Qutwub

Swali: Vitabu [vya Sayyid Qutwub] kama “Fiy Dhwilaal-il-Qur-aan” na “al-´Adalah al-Ijtimaaiyyah” na [Kitabu cha Abu Hamiyd al-Ghazaaliy] “Ihyaa´ ´Uluum-id-Diyn” vina mazuri na mabaya. Je, inajuzu kwangu kunukuu yale mazuri kutoka katika vitabu hivi ninapokuwa ninatoa mawaidha au kuandika kitu?

Jibu: Allaah Amekutosheleza kwa kutohitajia vitabu hivi. Kuna vitabu vya Salaf. Kuna vitabu vya wanachuoni na maimamu. Rejea kwavyo na jiepushe na vitabu ambavyo vimekosolewa au vinahitajia kuangaliwa. Achana navyo! Mazuri yaliyomo humo yanapatikana katika vitabu vyenye kuaminika na vinavyojulikana. Ama kuhusiana na mabaya yaliyomo humo, utakuwa umesalimika nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.4shared.com/audio/s1dSe7OS/___online.html
  • Imechapishwa: 18/12/2014