Jamaa´at-ut-Tabliygh hawatilii umuhimu kuzisahihisha ´Aqiydah. Kwa nini sisi katika vikao vyote hivi na miaka yote hii tunazungumzia kuhusu ni lazima kuusafisha Uislamu na malezi ya Kiislamu?

Mkuu wa Jamaa´at-ut-Tabliygh hatekelezi uwajibu huu kamwe. Badala yake amemuacha kila mtu katika kundi kuamini lile analotaka. Hili halijuzu katika Uislamu. Iko wapi dini ni nasaha? Iko wapi kuamrishana mema na kukatazana maovu?

Jamaa´at-ut-Tabliygh wakimuona mtu anaswali kwa madhehebu yake, hawamwambii kwamba Sunnah ni kuswali kwa njia hii. Hapana, wanasema kuwa hawataki kufarikisha waislamu.

Wanapomuona ndugu yao Muislamu anafanya Twawaaf kwenye kaburi, huenda wakashirikiana naye katika kufanya Twawaaf seuze tusiseme kumkataza. Kwa nini? Ni siasa ya kutaka kumfanya mtu awe katika mfumo na kundi. Da´wah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa namna hii? Allaah Anasema katika Qur-aan:

وَلَوْلَا أَن ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًا إِذًا لَّأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ

“Na lau kama hatukukuthibitisha, kwa hakika ungelikaribia kuelemea kwao kidogo. [Ungelifanya hivyo basi] hapo bila shaka Tungelikuonjesha [adhabu] maradufu ya uhai na [adhabu] maradufu [baada ya] kufa.” (17:74-75)

Huyu ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah Alimtahadharisha kuelemea kwa washirikina hata kama itakuwa kidogo. Je, sio shirki kufanya Twawaaf kwenye kaburi? Vipi tunaweza kukubali hili?

Siasa hii inaafikiana na makafiri na mfumo wao. Miongoni mwa siasa yao ni lengo zuri linasahilisha njia. Nikimfanya mtu kuingia katika Dini kwa njia kama hii, ninakuwa ni mwenye natambua mbele na tambo lingine kwa nyuma. Ni kweli kuwa nitamfanya kuswali, lakini Swalah yake na moyo wake umefungamana na shirki. Kwa nini hawatilii hawajali ´Aqiydah?

Tunajua sote – himdi zote ni Zake Allaah – hakuna tofauti yoyote kati ya makundi katika hili kwa kuwa Qur-aan imehifadhiwa – kwamba Da´wah ya Mitume ilikuwa ikianza kwa:

أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Mwabuduni Allaah na jiepusheni na miungu ya batili.” (16:36)

Je, Da´wah ya Jamaa´at-ut-Tabliygh inaanza kwa:

me ilikuwa ikianza kwa:

أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Mwabuduni Allaah na jiepusheni na miungu ya batili.”? (16:36)

وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ

“Na ndivyo hivyo Tumekufanyeni ummah wa kati na kati na adilifu ili muwe mashahidi juu ya watu.” (02:143)

Je, al-Ikhwaan al-Muslimuun huanza kwa hili? Je, Hizb-ut-Tahriyr huanza kwa hili? Kamwe! Kamwe! Kamwe! Kwa ajili hiyo ndio maana hakuna faika yoyote juu ya u-Hizbiyyah huu. Mola Wetu Anaweza kuwaongoza maelfu ya watu, kama sio mamilioni ya watu, kupitia mtu mmoja tu kwa kuwa anatembelea juu ya haki na njia iliyonyooka. Kwa ajili hiyo sisi tunashauri juu ya kwamba hakuna u-Hizbiyyah katika Uislamu na kwamba Waislamu ni Ummah mmoja. Allaah (´Azza wa Jalla) Amesema:

Ummah huu hauwezi kuwa bora maadamu haurejei kwa yale aliyokuwemo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Yule mwenye kuwafuata hawezi kujuta.

Mimi sifikirii kuwa wafuasi wengi wa makundi haya, ambapo vikundikundi vyao na vyama hatuvijui, si wenye Ikhlaasw. Hata hivyo ni wachache katika viongozi wao walio na Ikhlaasw. Sisemi kuwa wote hawana Ikhlaasw, lakini wengi wao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (540)
  • Imechapishwa: 18/12/2014