Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Suurah al-Baqarah na Aal ´Imraan zitakuja siku ya Qiyaamah zkimtetea mwenye nazo.”

Je, hii si dalili inayoonyesha kuwa zimeumbwa?

Jibu: Hapana. Zitakuja zikimtetea yule aliyekuwa akizisoma na kuzitendea kazi. Kwa kuwa ni Suurah ambazo ni hoja kutoka kwa Allaah. Mja ambaye alishikamana nazo na kuzitendea kazi, zitamtetea siku ya Qiyaamah. Allaah ni Muweza wa kuzifanya kwa umbile la sura kama jinsi kwa mfano Jibriyl alivyokuwa akijigeuza kwa umbile la mwanaadamu. Allaah ni Muweza wa kuvigeuza vitu kwa lengo la kuweza kuwasogelea waja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14331228.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015