Swali: Kikosi kidogo cha vijana wameacha kuwa wanaswali misikitini kwa sababu wanasema kuwa misikiti imegeuka ni kitu kama cha mapenzi kwa watawala. Pindi mtu anapotaka kuwanasihi wanasema kuwa wako katika haki na kwamba wako tayari kutupa changamoto ya kuomba laana ya Allaah imshukie mmoja katika sisi ambaye amekosea. Tutangamane nao vipi?

Jibu: Hili ndio janga ambalo tunatahadharisha. Huanza namna hii; wanataka kuwaka changamoto wengine kuomba laana ya Allaah imshukie yule aliyekosea. Baada ya hapo watazihalalisha damu zao, kuwatia waislamu ndani ya kufuru, kuwafanyia uasi watawala, kueneza fujo na mauaji. Baada ya hapo kunakuja khofu baada ya amani na mengine mengi.

Naapa kwa Allaah! Kauli yao mbiu hii si jengine isipokuwa batili tupu. Haya ndio madhehebu ya Khawaarij. Hawa ndio wale Khawaarij ambao waliwakufurisha Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakamkufurisha khaliyfah ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh). Watu hawa ni watu wa batili na wapotevu.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath-ur-Rahiym al-Waduud, uk. 259-260
  • Imechapishwa: 28/06/2020