Hivi kweli leo kuna haja ya kuuliza juu ya picha?

Swali: Ni ipi hukumu ya picha?

Jibu: Ni jambo lililofichikana kwenu juu ya hukumu ya picha pamoja na kwamba kuna Hadiyth nyingi Swahiyh zilizo wazi zinazokataza na kutoa matishio ya adhabu kwa mwenye kufanya hivo? Vilevile kumeandikwa makala na vitabu. Jambo hili limekuwa wazi. Halina utatizi ndani yake. Isitoshe kuna fataawaa za wanachuoni zilizochapishwa. Kwa sasa hakuna haja ya kuulizia hilo tena. Mambo yamekuwa wazi juu ya kwamba ni haramu na haijuzu. Isipokuwa wakati wa dharurah tu. Kukiwepo dharurah itafanywa kiasi cha dharurah itakavokuwa. Kuhusiana na picha za sanaa, kumbukumbu na mfano wa hizo haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-11-7.mp3
  • Imechapishwa: 27/08/2020