Swali: Watu wakikaa nyumbani kwa maiti kwa ajili ya kutoa pole kisha na mimi nikaenda kutoa pole nitakuwa ni mwenye kupata dhambi?

Jibu: Hili litapelekea wewe kuwapa nguvu na kukubaliana na wanayoyafanya. Bora zaidi nenda wakati ambapo hawakukusanyika. Unaweza kwenda kumpa pole mfiliwa kinyume na wakati ambapo hawakukusanyika. Nenda ukutane naye msikitini, kazini, idara na kwenginepo. Tenga nafasi uitumie fursa hiyo kumpa pole mfiliwa mbali na mikusanyiko hii. Vilevile unaweza kuwasiliana naye kwa simu na kumpa pole. Malengo yatakuwa yamefikiwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (35) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1430-11-7.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020