Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika sisi Mitume haturithiwi. Hatukuacha mirathi.” Ahmad (02/463)
Hii ni hekima ya Allaah (´Azza wa Jall). Kwa sababu lau wangelikuwa wanarithiwa angelisema mwenye kusema kwa vile watu hawa ndio wamekuja na ujumbe basi tunatafuta wafalme wenye kuwarithi baada yao. Allaah (´Azza wa Jall) akakataza hilo. Mitume hawarithiwi. Wanavoviacha inakuwa swadaqah. Wanapewa wale wenye kuiistahiki.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/205)
- Imechapishwa: 19/02/2023