Subira na matarajio wakati wa msiba

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha mwanaume amwambie mama wa mtoto ambaye amefiwa amwambia yafuatayo:

“Awe na subira na ataraji malipo kutoka kwa Allaah.”

Bi maana ataraji ujira kutoka kwa Allaah kutokana na kusubiri kwake. Kuko watu ambao wanasubiri lakini hata hivyo hawataraji malipo kwa Allaah. Mtu anasubiri katika msiba na hana nyongo, lakini hata hivyo hataraji malipo kutoka kwa Allaah. Kwa hivyo anakuwa ni mwenye kupitwa na ujira mwingi. Upande mwingine akiwa ni mwenye subira na wakati huohuo akataraji malipo kutoka kwa Allaah, kwa msemo mwingine anakusudia kwa kusubiri kwake kupewa thawabu na ujira na Allaah, huku ndio kutaraji malipo kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/207)
  • Imechapishwa: 19/02/2023