Hello wakati wa kuitikia salamu

Swali: Je, mtu anapata dhambi kwa kusema “hello” wakati wa kuitikia salamu?

Jibu: Ni kwenda kinyume na Sunnah. Kilicho cha wajibu ni kuitikia salamu kwa kusema:

وعليكم السلام

“Nanyi amani ya Allaah iwe juu yenu.”

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٍ فَحَيُّوا بِأَحْسَنَ مِنْهَا أَوْ رُدُّوهَا

“Mtapoamkiwa kwa maamkizi yoyote, basi itikieni kwa yaliyo mazuri zaidi kuliko hayo au yarudisheni hayo hayo.” (04:86)

Kwa hivyo afunzwe na kuelekezwa katika kheri.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23938/حكم-رد-السلام-بقول-هلا-او-مرحبا
  • Imechapishwa: 01/08/2024