Swali: Ni lazima kwa mwanamke kufunika uso wake hata kama uso wake ni mbaya?

Jibu: Haijalishi kitu. Isipokuwa hapana vibaya kwa wanawake wazee waliokatika hedhi wasiotamani ndoa na wala hawajipodoi. Kuhusu wengine kunaweza kuwepo utata. Kila chenye kutupwa kina mwenye kukiokota; wanawake kama hao wanaweza kuwatia kwenye mtihani baadhi ya watu. Isitoshe ubaya hauna kikomo sahihi; mwanamke anaweza kuwa mbaya kwa mujibu wa watu fulani na mrembo kwa mujibu wa wengine.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23937/هل-يجب-ستر-وجه-المراة-ولو-كان-قبيحا
  • Imechapishwa: 01/08/2024