Ibn Baaz kuhusu mwanamke kutoka kwenda sokoni

Swali: Leo wanawake kutoka kwenda kwenye masoko imekuwa ni jambo la kawaida.

Jibu: Hapana vibaya ikiwa ni kutokana na haja yake. Au akatoka kununua au kuuza. Hapana vibaya kwa sharti atoke hali ya kuwa amejisitiri.

Swali: Vipi kuhusu mwanamke anayetoka sana na daima?

Jibu: Hapana vibaya ikiwa ni kutokana na haja yake. Lakini ikiwa hakuna haja mume wake amtatulie haja zake.

Swali: Anatoka kwa ajili ya kukamilisha baadhi ya mambo?

Jibu: Si kila mmoja anafaa kutoka kununua haja.

Swali: Ni lazima atoke na Mahram?

Jibu: Hapana. Mahram ni safarini. Hahitaji Mahram. Akiwa ni mwaminifu hahitaji Mahram.

Swali: Baadhi ya wanawake wanatoka na madereva?

Jibu: Haifai kwenye gari. Ni lazima awepo mtu wa tatu. Lakini ikiwa anatembea kwa miguu yake hahitaji kuwa na Mahram. Asiende na dereva, ni lazima mwanamke huyo awe na mtu wa tatu ima mwanamke mwenzie, mwanaume au zaidi ya hapo ili kuondosha mashaka.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23920/حكم-كثرة-خروج-النساء-للاسواق
  • Imechapishwa: 01/08/2024