Swali: Baadhi ya watu wanapopatwa na jambo basi husema:

لا حول

“Hapana uwezo wa kutikisika.”

na wala hawakamilishi kwa kusema:

لا حول ولا قوة إلا بالله

“Hapana uwezo wa kutikisika wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”?

Jibu: Hapana, wakamilishe kwa kusema:

لا حول ولا قوة إلا بالله

“Hapana uwezo wa kutikisika wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumwambia Abu Muusa:

“Je, nisikujuze hazina miongoni mwa hazina za Pepo?

لا حول ولا قوة إلا بالله

“Hapana uwezo wa kutikisika wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23697/حكم-قول-لا-حول-فقط-دون-بقيتها
  • Imechapishwa: 06/04/2024