Swali: Kuna mlinganizi mmoja anasema kwamba Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:
“Wanawake ni wapungufu wa akili na dini”
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema hivi wakati ambapo alikuwa anatania na wanawake na hakusema hivi akimaanisha hakika”.” Je, maneno yake haya yana ukweli wowote ndani yake?
Jibu: Maneno haya ni batili. Si kwamba yana ukweli wowote ndani yake, bali ni maneno ya batili. Maneno haya yanapingana na Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawa ndio wale wanaodaiwa kuwa ni katika watetezi wa mwanamke. Wanataka kumfanya mwanamke ni kama mwanaume. Wanataka kubadilisha maumbile ambayo Allaah Amewaumba watu kwayo:
وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ
“Na mwanamme si kama mwanamke.” (03:36)
Haya ni maneno batili. Hayasemi mwanachuoni. Ima yanasema mjinga au mpotevu na tunaomba kinga kwa Allaah.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin al-Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: alfawzan.af.org.sa
- Imechapishwa: 22/05/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)