Haya hayakusemwa na wanachuoni – yamesemwa na mjinga au mpotevu

Swali: Kuna mlinganizi mmoja anasema kwamba Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

“Wanawake ni wapungufu wa akili na dini”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema hivi wakati ambapo alikuwa anatania na wanawake na hakusema hivi akimaanisha hakika”.” Je, maneno yake haya yana ukweli wowote ndani yake?

Jibu: Maneno haya ni batili. Si kwamba yana ukweli wowote ndani yake, bali ni maneno ya batili. Maneno haya yanapingana na Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawa ndio wale wanaodaiwa kuwa ni katika watetezi wa mwanamke. Wanataka kumfanya mwanamke ni kama mwanaume. Wanataka kubadilisha maumbile ambayo Allaah Amewaumba watu kwayo:

وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ

“Na mwanamme si kama mwanamke.” (03:36)

Haya ni maneno batili. Hayasemi mwanachuoni. Ima yanasema mjinga au mpotevu na tunaomba kinga kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin al-Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: alfawzan.af.org.sa
  • Imechapishwa: 22/05/2022