Swali: Je, mtu afanye Tayammum kwa ajili ya swalah ya Fajr akihitajia kuoga na asiweze kutumia maji kutokana na ukali wa baridi na kusiwepo namna ya kupasha maji? Ni ipi hukumu ya ambaye amefanya hivo?
Jibu: Akiwa maeneo ambapo hawezi kuyapasha maji au yuko mahali ambapo anaweza kufanya mkaa akapasha maji kwa ajili ya kujitwahirisha mwa maji moto na wakati huohuo akachelea juu ya nafsi yake, basi ataswali kwa Tayammum na hapana vibaya kwake. Allaah (Ta´ala) amesema:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Na yale niliyokuamrisheni basi yaendeeni kiasi muwezavyo.”
Imethibiti kwamba ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa katika vita iliokuwa na minyororo na akapatwa na janaba. Ilikuwa katika usiku wenye baridi kali na hakuoga. Bali akatawadha na akafanya Tayammum na akawaswalisha watu. Wakati alipofika kutoka vitani akamuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasema kwamba alichelea juu ya nafsi yake na akafasiri maneno ya Allaah (Subhaanah):
وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا
“Wala msiziue nafsi zenu. Hakika Allaah ni Mwenye kuwahurumia.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatabasamu na wala hakusema kitu na wala hakumwamrisha kurudia. Hivyo ikajulisha kwamba ni udhuru unaokubalika katika Shari´ah.
[1] 64:16
[2][2] 04:29
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/200)
- Imechapishwa: 03/09/2021
Swali: Je, mtu afanye Tayammum kwa ajili ya swalah ya Fajr akihitajia kuoga na asiweze kutumia maji kutokana na ukali wa baridi na kusiwepo namna ya kupasha maji? Ni ipi hukumu ya ambaye amefanya hivo?
Jibu: Akiwa maeneo ambapo hawezi kuyapasha maji au yuko mahali ambapo anaweza kufanya mkaa akapasha maji kwa ajili ya kujitwahirisha mwa maji moto na wakati huohuo akachelea juu ya nafsi yake, basi ataswali kwa Tayammum na hapana vibaya kwake. Allaah (Ta´ala) amesema:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Na yale niliyokuamrisheni basi yaendeeni kiasi muwezavyo.”
Imethibiti kwamba ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa katika vita iliokuwa na minyororo na akapatwa na janaba. Ilikuwa katika usiku wenye baridi kali na hakuoga. Bali akatawadha na akafanya Tayammum na akawaswalisha watu. Wakati alipofika kutoka vitani akamuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akasema kwamba alichelea juu ya nafsi yake na akafasiri maneno ya Allaah (Subhaanah):
وَلَا تَقْتُلُوا أَنفُسَكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِكُمْ رَحِيمًا
“Wala msiziue nafsi zenu. Hakika Allaah ni Mwenye kuwahurumia.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatabasamu na wala hakusema kitu na wala hakumwamrisha kurudia. Hivyo ikajulisha kwamba ni udhuru unaokubalika katika Shari´ah.
[1] 64:16
[2][2] 04:29
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/200)
Imechapishwa: 03/09/2021
https://firqatunnajia.com/hawezi-kutumia-maji-katika-wudhuu-kutokana-na-ukali-wa-baridi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)