Inajuzu kwa wanandoa kuoshana wanapokufa?

Jibu: Inafaa kwa mume kumwosha mke wake atapokufa kama ambavyo inafaa kwa mke kumwosha mume wake atapokufa. Imesimuliwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):

“Lau utakufa kabla yangu basi nitakuosha.”[1]

Vilevile Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) aliusia aoshwe na mke wake Asmaa´ bint Umays (Radhiya Allaahu ´anhaa).

[1] Ahmad (06/228) na Ibn Maajah (1465).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/211-212)
  • Imechapishwa: 03/09/2021