Swali: Nilifanyiwa operesheni mgongoni mwangu na mimi naweza kutawadha lakini kwa uzito. Siku miongoni mwa siku niliota na sikuweza kuoga ili donda la operesheni lisije kuathirika. Je, inanitosha kufanya Tayammum? Je, ni lazima nitawadhe baada ya kuoga au nifanye nini katika hali kama hii?
Jibu: Ni lazima kwa muislamu kumcha Allaah kiasi awezacho katika hali zake zote. Allaah (Subhaanah) amesema:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yale niliyokukatazeni basi jiepusheni nayo na yale niliyokuamrisheni basi yaendeeni kiasi muwezavyo.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Ikiwa mgonjwa hawezi kutawadha wala kuoga basi kunamtosha kufanya Tayammum. Allaah (Subhaanah) amesema:
وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ
”Mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu akitoka chooni au mmewagusa wanawake, kisha hamkupata maji, basi fanyeni Tayammum kwa ardhi ilio safi panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”[2]
Ambaye ameshindwa kutawadha au kuoga basi hukumu yake ni kama yule ambaye amekosa maji. Akiweza kutawadha pasi na kuoga basi atatawadha na kufanya Tayammum badala ya kuoga. Kama ilivyotangulia katika maneno Yake (Ta´ala):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[3]
[1] 64:16
[2] 05:06
[3] 64:16
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/196)
- Imechapishwa: 03/09/2021
Swali: Nilifanyiwa operesheni mgongoni mwangu na mimi naweza kutawadha lakini kwa uzito. Siku miongoni mwa siku niliota na sikuweza kuoga ili donda la operesheni lisije kuathirika. Je, inanitosha kufanya Tayammum? Je, ni lazima nitawadhe baada ya kuoga au nifanye nini katika hali kama hii?
Jibu: Ni lazima kwa muislamu kumcha Allaah kiasi awezacho katika hali zake zote. Allaah (Subhaanah) amesema:
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yale niliyokukatazeni basi jiepusheni nayo na yale niliyokuamrisheni basi yaendeeni kiasi muwezavyo.”
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Ikiwa mgonjwa hawezi kutawadha wala kuoga basi kunamtosha kufanya Tayammum. Allaah (Subhaanah) amesema:
وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ
”Mkiwa wagonjwa au mko safarini au mmoja wenu akitoka chooni au mmewagusa wanawake, kisha hamkupata maji, basi fanyeni Tayammum kwa ardhi ilio safi panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”[2]
Ambaye ameshindwa kutawadha au kuoga basi hukumu yake ni kama yule ambaye amekosa maji. Akiweza kutawadha pasi na kuoga basi atatawadha na kufanya Tayammum badala ya kuoga. Kama ilivyotangulia katika maneno Yake (Ta´ala):
فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ
”Mcheni Allaah muwezavyo.”[3]
[1] 64:16
[2] 05:06
[3] 64:16
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/196)
Imechapishwa: 03/09/2021
https://firqatunnajia.com/ameota-na-hawezi-kutumia-maji-kwa-sababu-ya-ugonjwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)